• HABARI MPYA

  Thursday, April 28, 2016

  DIEGO SIMEONE AFUNGIWA MECHI ZOTE ZILIZOBAKI LA LIGA

  KOCHA Mkuu wa Atletico Madrid, Diego Simeone (pichani kulia) amefungiwa kukaa kwenye benchi kwa mechi zote tatu zilizobaki za timu yake katika Ligi Kuu ya Hispania, La Liga kumalizia msimu.
  Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 45 amepewa adhabu hiyo baada ya mpira kurushwa uwanjani katika mchezo wa Jumamosi, timu yake ikishinda 1-0 dhidi ya Malaga.
  Picha za Televisheni zinaonyesha kwamba mpira huo ulipokuwa nje katika himaya ya kijana muokota mpira, ukarushwa uwanjani kutoka eneo la benchi la Atletico Madrid na kuvuruga shambulizi la Malaga. 
  Na kwa kuwa mpira uliporushwa kutoka eneo la benchi la ufundi la Atletico - sheria zinambana kocha kwamba ndiye wa kuwajibishwa na Simeone amedhibiwa. 
  Kocha huyo wa Atletico alipandishwa jukwaani na refa Antonio Mateu Lahoz baada ya ripoti kusema hakumtaja aliyerusha mpira uwanjani.
  Madrid inalingana kwa pointi Barcelona kileleni mwa msimamo wa La Liga, wakati Real Madrid inazidiwa pointi moja katika nafasi ya tatu.
  Simeone sasa hatakaa benchi katika mechi dhidi ya Rayo Vallecano, Levante na Celta Vigo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DIEGO SIMEONE AFUNGIWA MECHI ZOTE ZILIZOBAKI LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top