• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 21, 2016

  YANGA YAPEWA WAANGOLA KUWANIA MAKUNDI YA KOMBE LA SHIRIKISHO

  MECHI ZA MCHUJO WA KUWANIA KUCHEZA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO 
  Yanga SC (Tanzania) Vs Sagrada Esperanca (Angola)
  MO Bejaia (Algeria) Vs Esperance (Tunisia)
  Stade Malien (Mali) Vs FUS Rabat (Morocco)
  Etoile Du Sahel (Tunisia) Vs CF Mounana (Gabon)
  TP Mazembe (DRC) Vs Stade Gabesien (Tunisia)
  Ahli Tripoli (Libya) Vs Misr Makassa (Misri)
  El Merreikh (Sudan) Vs Kawkab (Morocco)
  Mamelodi Sundowns (Africa Kusini) Vs Medeama (Ghana)
  (Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Mei 6 na 8 na marudiano kati ya Mei 17 na 18, 2016)

  Sagrada Esperanca na ilianzishwa Desemba 22, mwaka 1976 na Serikali ya Angola, ila kwa sasa inamilikiwa na kampuni ya madini ya Almasi, Endiama, ambao pia ni wadhamini wakuu

  Na Prince Akbar, CAIRO
  YANGA SC itamenyana na Sagrada Esperanca ya Angola kuwania kuingia kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, mechi ya kwanza ikichezwa Dar es Salaam kati ya Mei 6 na 8 na marudiano ugenini kati ya mei 17 na 18.
  Jina la wapinzani hao wa Yanga linatokana na rais wa kwanza wa Angola, Agostinho Neto, maarufu kwa jina la utani Sagrada Esperanca na ilianzishwa Desemba 22, mwaka 1976 na Serikali ya Angola.
  Baadaye ikawa inamilikiwa na kampuni ya madini ya Almasi, Diamang (sasa Endiama), ambao wanabakia kuwa wadhamini wakuu.
  Yanga jana ilitolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa mabao 2-1 na Al Ahly Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora.
  Al Ahly imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya awali kulazimisha sare ya 1-1 Uwanja wa Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.
  Abdallah Said aliifungia Ahly bao la ushindi dakika ya sita ya muda wa nyongeza baada ya kukamilika kwa dakika 90 za kawaida za mchezo akimalizia krosi ya  Walid Soliman kutoka upande wa kushoto.
  Al Ahly walitangulia kupata bao katika mchezo wa leo kupitia kwa kiungo Hossam Ghaly aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Ahmed Fathi dakika ya 52.
  Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Dombo Ngoma akaisawazishia Yanga dakika ya 57 kwa kichwa akimalizia krosi nzuri ya beki wa kulia Juma Abdul.
  Kwa Yanga, hii ni mara ya pili kufikia hatua hiyo baada ya mwaka 2007. Mwaka huo Yanga ilifungwa 3-0 na Esperance ya Tunisia katika hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kutoa sare 0-0 Mwanza.
  Katika kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho na ilitolewa na El Merreikh ya Sudan, ikitoa sare ya 0-0 Mwanza na kufungwa 2-0 Khartoum. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA YAPEWA WAANGOLA KUWANIA MAKUNDI YA KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top