• HABARI MPYA

  Wednesday, April 27, 2016

  MWANDISHI WA DIMBA AWA OFISA HABARI TFF

  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemteua Alfred Lucas kuwa Afisa Habari na Mawasiliano mpya wa shirikisho kuanzaia leo Aprili 27, 2016.
  Alfred anachukua nafasi ya Baraka Kizuguto aliyehamishiwa katika Kurugenzi ya Mashindano kuwa Afisa Mashindano na Meneja wa Mifumo pepe ya Usajili (TMS).
  Alfred ana uzoefu kutoka vyombo mbalimbali alivyovitumikia kama mwandishi wa habari na mhariri, likiwemo gazeti la Dimba lilimuinua kabla ya kwenda magazeti mengine.
  Kadhalika Alfred kitaaluma amesomea uandishi wa habari, uhusiano wa kimataifa na diplomasia pamoja na lugha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWANDISHI WA DIMBA AWA OFISA HABARI TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top