• HABARI MPYA

    Friday, April 29, 2016

    TFF KUSIKILIZA RUFAA ZA GEITA KESHO, KESI ZA AKINA BOCCO, NGOMA 'ZAPIGWA KALENDA'

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIKAO cha Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kitafanyika Jumamosi Aprili 30, 2016 kuanzia saa 4.00 asubuhi kwenye ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Ilala mjini Dar es Salaam.
    Kikao hicho kitajadili rufaa za timu, makocha, viongozi na wachezaji waliokata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Nidhamu baada ya kamati hiyo kuwatia hatiani na kuwaadhibu kwa makosa ya kupanga matokeo ya michuano ya Ligi Daraja la Kwanza.
    Rufaa zitakazojadiliwa kwenye kikao hicho ni za Geita Gold, kocha Msaidizi wa timu hiyo, Choki Abeid, kipa wa timu hiyo, Denis Richard Dioniz,  Katibu wa Chama cha Mpira Soka Tabora (TAREFA), Fatel Rhemtullah, REFA Saleh Mang’ola wa Dodoma, Polisi Tabora, JKT Oljoro FC ya Arusha na Mwenyekiti wa TAREFA, Yusufu Kitumbo.
    Aidha, Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya TFF kilichopangwa kufanyika Jumapili, Mei Mosi 2016, kimeahirishwa hadi Jumanne Mei 3, mwaka huu.
    Sababu za kuahirisha kikao hicho ni kwamba baadhi ya wajumbe wamepata udhuru hivyo wangeshindwa kuhudhuria kikao hicho kitakachofanyika mjini Dar es Salaam kupitia mashauri mbalimbali yaliyowasilishwa.  
    Kikao hicho kinatarajiwa kujadili kesi za wachezaji John Bocco (Azam FC), Shomari Kapombe (Azam FC), Aishi Manula (Azam FC), Amissi Tambwe (Yanga SC), Donald Ngoma (Yanga SC), Paulo Jinga (JKT Rwamkoma FC) na Kipre Tchetche (Azam FC).
    Wengine ni Abel Katunda (Transit Camp), Zephlyn Laurian (JKT Rwamkoma FC), Idrisa Mohamed (JKT Rwamkoma), Mganaga Kitambi (Daktari wa Coastal Union), Herry Chibakasa (Friends Rangers),  Ismail Nkulo (Polisi Dodoma), Said Juma (Polisi Dodoma), Idd Selaman (Polisi Dodoma), Edward Amos (Polisi Dodoma) na kocha Stewart Hall (Azam FC).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF KUSIKILIZA RUFAA ZA GEITA KESHO, KESI ZA AKINA BOCCO, NGOMA 'ZAPIGWA KALENDA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top