• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 24, 2016

  REAL MADRID HATARINI KUMKOSA BENZEMA DHIDI YA MAN CITY

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa, Karim Benzema anaweza kukosekana katika kikosi cha Real Madrid kitakachosafiri kwenda England kumenyana na Manchester City katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne.
  Hiyo inafuatia mpachika mabao huyo kuumia katika mchezo wa La Liga jioni ya Jumamosi dhidi ya Rayo Vallecano, Real Madrid ikishinda 3-2.
  Benzema alitolewa dakika ya 42 ya mchezo huo Uwanja wa Vallecas, nafasi yake ikichukuliwa na Lucas Vazquez. Vazquez akafunga baada ya kutokea benchi Real ikitoka nyuma kwa mabao 2-0 na kushinda 3-2.
  Karim Benzema akizungumza na kocha wa Real Madrid, Mfaransa mwenzake Zinedine Zidane baada ya kushindwa kuendelea na mchezo Jumamosi PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Mfaransa huyo aliumia goti lake wa kulia, na sasa anawaachia hofu mashabiki wa timu yake kuelekea Nusu Fainali ya Kwanza ya michuano ya Ulaya Uwanja wa Etihad katikati ya wiki ijayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REAL MADRID HATARINI KUMKOSA BENZEMA DHIDI YA MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top