• HABARI MPYA

    Monday, April 25, 2016

    'VIBABU' WAWILI WAORODHESHWA KIKOSI CHA CHIPOLOPOLO CHA COSAFA

    MSHAMBULIAJI Christopher Katongo na kiungo Isaac Chansa wamerejeshwa kwenye kikosi cha Zambia baada ya kocha George Lwandamina kutaja kikosi chake cha awali leo kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) 2016.
    Wakongwe hao wawili waliondolewa kwenye kikosi cha mwisho cha wachezaji 22 kilichotajwa na Chama cha Soka Zambia (FAZ).
    Katongo na Chansa wa Green Buffaloes na Zanaco wamerejeshwa kwenye kikosi cha Zambia baada ya kung'ara wakiwa na Chipolopolo kwenye michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mapema mwaka huu nchini Rwanda, ambako waliifikisha timu hiyo Robo Fainali na pia kufanya vizuri katika michezo ya Kundi E kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 Africa dhidi ya Kongo iliyoisha kwa sare ya 1-1 nyumbani na ugenini.

    Mkongwe Christopher Katongo amerejeshwa kwenye kikosi cha Zambia kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) 2016

    Lwandamina pia amemuita kiungo Jacob Ngulube ambaye amekuwa na mwanzo mzuri katika klabu yake mpya, Nkana tangu ajiunge na mabingwa hao mara 12 wa Zambia kutoka Mufulira Wanderers.
    Ngulube amekuwa na mchango mkubwa kwa Nkana ambayo haiijapoteza mechi na imekuwa ikiongoza Ligi Kuu ya Zambia tangu mwanzoni mwa Machi, akifunga mabao matatu katika mechi sita.
    Wakati huo huo: Kikosi cha wachezaji 25 wa Zambia kinaanza mazoezi Mei 1 katika kambi yake mjini Ndola kwa maandalizi ya awali ya COSAFA 2016, ambayo itafanyika Namibia kwa mabingwa watetezi kuanzia Juni 11 hadi 25.
    Kikosi hicho kinaundwa na makipa; Jacob Banda (Zesco United), Danny Munyao (Red Arrows) na Racha Kola (Zanaco).
    Mabeki; Boyd Mkandawire (Napsa Stars), Benedict Chepeshi (Red Arrows), Dauti Musekwa (Zesco United), Buchizya Mfune , Adrian Chama (both Green Buffaloes), George Chilufya (Zanaco) na Donashano Malama (Nkana).
    Viungo; Jacob Ngulube (Nkana), Jack Chirwa (Green Buffaloes), Benson Sakala (Power Dynamos), Paul Katema (Red Arrows), Isaac Chansa, Salulani Phiri ,Charles Zulu (all Zanaco), Spencer Sautu, Mwila Phiri (both Green Eagles) na Clatous Chama (Zesco United).
    Washambuliaji; Adamson Mulawo (Green Eagles), Festus Mbewe (Red Arrows), Patson Daka (Power Dynamos), Conlyde Luchanga (Lusaka Dynamos) na Christopher Katongo (Green Buffaloes).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: 'VIBABU' WAWILI WAORODHESHWA KIKOSI CHA CHIPOLOPOLO CHA COSAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top