• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 25, 2016

  SAMATTA ATOLEWA BAADA YA KIPINDI CHA KWANZA GENK IKILALA 2-1 NYUMBANI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta (pichani kulia) amecheza kwa dakika 45 tu za kwanza, wakati timu yake, KRC Genk ikifungwa 2-1 na Gent katika mchezo wa mchujo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji, maarufu kama Pro League usiku wa leo tena Uwanja wa nyumbani, Cristal Arena mjini Genk.
  Samatta alitolewa baada ya kumalizika kipindi cha kwanza, akimpisha mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis ambaye wamekuwa wakipokezana siku zote.
  Wakati Samatta anatoka timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, Genk wakitangulia kwa bao la Leon Bailey dakika ya 16, kabla ya Laurent Depoitre kuwasawazishia wageni dakika ya 23. 
  Renato Neto akaifungia Gent bao la ushindi kwa penalti dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimu kwa dakika 90 za kawaida za mchezo.
  Samatta leo alikuwa akicheza mechi ya 11 tangu ajiunge na Genk Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya DRC, akiwa amefunga mabao nne. 
  Samatta alifunga bao moja katika ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji SV Zulte-Waregem mwishoni mwa wiki baada ya awali kufunga katika ushindi wa 4-0 na 4-1 dhidi ya KV Oostende na 3-2 dhidi ya Club Brugge.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA ATOLEWA BAADA YA KIPINDI CHA KWANZA GENK IKILALA 2-1 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top