• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 27, 2016

  TYSON FURY AVUA NGO KUMUONYESHA 'MANYAMA UZEMBE' KLITSCHKO

  BONDIA Tyson Fury leo amevua fulana yake kuonyesha kitambi chake huku akimkandia mpinzani wake, Wladimir Klitschko kwa kujiruhusu kupigwa na 'manyama uzembe' kama yeye.
  Kituko hicho alikifanya katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea pambano lao la marudiano la uzito wa juu baadaye mwaka huu.
  Fury atatetea mataji yake ya dunia ya WBA na WBO aliyoyatwaa kwa kumshinda Klitschko mjini Dusseldorf, Ujerumani Novemba mwaka jana katika pambano litakalofanyika ukumbi wa Manchester Arena Julai 9.
  "Mtu mnene - ambaye amekupiga wewe. Aibu yako,"alisema Fury akiwa amevua fulana huku akimgeukia Klitschko katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo. 
  Tyson Fury akiwa amevua fulana yake kumuonyesha manyama yake mpinzani wake Wladimir Klitschko wakati wa Mkutano wa kutangaza pambano lao la marudiano litakalofanyika ukumbi wa Manchester Arena Julai 9, mwaka huu  PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TYSON FURY AVUA NGO KUMUONYESHA 'MANYAMA UZEMBE' KLITSCHKO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top