• HABARI MPYA

  Tuesday, April 26, 2016

  TAIFA STARS KUMENYANA NA HARAMBEE NAIROBI MEI 29

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na Kenya, Harambee Stars mwezi ujao.
  Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utachezwa mjini Nairobi, Kenya Mei, 29 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote mbili kujaindaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika mapema mwezi Juni, 2016.
  TFF kwa kushirkiana na FKF zimekubaliana kuwepo kwa mchezo huo wa kirafiki, utakotumika kama sehemu za maandalizi kwa timu zote kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 mwezi Juni.
  Kikosi cha Taifa Stars mwaka huu

  Kikosi cha Taifa Stars kianchonolewa na kocha mkuu, Charles Boniface Mkwasa kinatarajiwa kuingia kambini mapema Mei, mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuwakabili Misri katika uwanja wa Taifa mjini Dra es Salaam Juni 04, 2016.
  Stars inajianda na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika mwaka 2017 nchini Gabon dhdi ya Misri utakaochezwa Juni 4, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS KUMENYANA NA HARAMBEE NAIROBI MEI 29 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top