• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 23, 2016

  FARID ATUA SALAMA HISPANIA TAYARI KUJARIBU BAHATI LA LIGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WINGA wa Azam FC, Farid Mussa amewasili salama nchini Hispania kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa katika klabu za La Liga.
  Akizungumza kutoka Madrid, Hispania, Farid ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kwamba amepokewa vizuri na wakala wake na leo anatarajia kupewa ratiba nzima.
  “Ndiyo kwanza jamaa nimekutana naye sasa hivi, nadhani nitakwenda kupumzika na kesho (leo) ndiyo nitajua ratiba nzima,”amesema.
  Kwa mujibu wa taarifa za awali, Farid atafanya majaribio klabu za Union Deportiva Las Palmas, maarufu kama Las Palmas yenye maskani yake Las Palmas de Gran Canaria na Athletic ya Bilbao.
  Farid Mussa akiwa na wakala wake baada ya kutua Hispania jana usiku

  Farid amewasili Hispania akitoka kuichezea klabu yake, Azam FC katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Esperance walioshinda 3-0 mjini Tunis Jumanne.
  Na Farid aliyefunga bao la kwanza na kuseti la pili lililofungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’ katika mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam Azam FC ikitoka nyuma kwa 1-0 na kushinda 2-1 anatarajiwa kuwa Hispania kwa wiki mwezi mmoja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FARID ATUA SALAMA HISPANIA TAYARI KUJARIBU BAHATI LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top