• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 27, 2016

  BOCCO, NGOMA NA TAMBWE 'KIZIMBANI' TFF

  Kesi ya Nahodha wa Azam FC, John Bocco itajadiliwa katika kikao cha Kamati ya Nidhamu Jumapili
  WASHAMBULIAJI John Bocco wa Azam FC na Donald Ngoma wa Yanga wanatarajiwa kujadiliwa katika Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jumapili ya Mei Mosi, mwaka huu mjini mjini Dar es salaam.
  Kamati hiyo ya Nidhamu itapitia mashauri mbalimbali yaliyowasilishwa.  
  Mbali na Bocco na Ngoma, wengine ambao kesi zao sitasikilizwa katika kikao hicho ni Shomari Kapombe wa Azam FC, Aishi Manula (Azam FC), Amissi Tambwe (Yanga SC), Paulo Jinga (JKT Rwamkoma FC), Kipre Tchetche (Azam FC) na Abel Katunda (Transit Camp).
  Wamo pia Zephlyn Laurian (JKT Rwamkoma FC), Idrisa Mohamed (JKT Rwamkoma), Dk Mganaga Kitambi (Daktari wa Coastal Union), Herry Chibakasa (Friends Rangers), Ismail Nkulo (Polisi Dodoma), Said Juma (Polisi Dodoma), Idd Selaman (Polisi Dodoma), Edward Amos (Polisi Dodoma) na  Stewart Hall (Kocha wa Azam FC).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BOCCO, NGOMA NA TAMBWE 'KIZIMBANI' TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top