• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 25, 2016

  TFF YAITAKA YANGA KUFANYA UCHAGUZI JUNI 5

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU bingwa ya Tanaznia, Yanga SC itafanya uchaguzi wake Mkuu Juni 5, mwaka huu. Hayo ni maagizo ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
  Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Wakili Aloyce Komba amesema mchakato mzima wa uchaguzi wa Yanga utakuwa ndani ya siku 33 na mchakato unatarajiwa kuanza rasmi Mei 3, 2016.
  Komba amesema jukumu lao Kamati ya Uchaguzi TFF  ni kusimamia na kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo unafanyika katika hali ya demokrasia.
  wakilia Komba ametaja ratiba ya mchakato wa Uchaguzi katika Yanga kuwa ni Mei 3, 2016 Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, atatangaza mchakato wa kulabu ya Yanga, nafasi zinazogombewa na kubandika kwenye mbao za matangazo.
  Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Yanga SC, Yussuf Manji 

  Mei 04-9, 2016 – Kuanza kuchukua fomu za kugombea na mwisho wa kurudisha fomu kwa wagombea.
  Mei 10, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF itakaa kikao cha mchujo wa awali  wa wagombea na kuandika barua za kuwajulisha wagombea juu ya mchujo wa awali.
  Mei 11, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF itachapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo orodha ya awali ya wagombea.
  Mei 12-13, 2016 Kipindi cha kupokea na kuweka pingamizi kwa wagombea wote.
  Mei 14-15, 2016 Kamagi ya Uchaguzi TFF itapitia pingamizi zote na kufanya usajili wa wagombea.
  Mei 16, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF itatangaza na kubandika kwenye mbao za matangazo matokeo ya awali ya usahili.
  Mei 17, 2016 Sekretarieti kuwasilisha masuala ya kimaadili kwenye Kamati ya Maadili ya TFF.
  Mei 18-19, 2016 Kamati ya Maadili TFF itapokea, kusikiliza na kutolea maamuzi ya kamati ya maadili.
  Mei 20, 2016 Kamati ya Maadili ya TFF itatangaza maamuzi ya kamati.
  Mei 21-22, 2016 Kipindi cha kukata Rufaa kwa maamuzi ya masuala ya Kimaadili kwenye kamati ya Rufaa ya Maadili TFF.
  Mei 23, 2016 Kamati ya Maadili tff itasikiliza rufaa za kimaadili.
  Mei 24, 2016 Kamati ya Rufaa ya Maadili itatoa maamuzi ya Rufaa.
  Mei 25-26, 2016 Kipindi cha kukata Rufaa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi kwenye kamati ya Rufaa ya Uchaguzi TFF.
  Mei 27-28, 2016 Rufaa kusikilizwa na kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
  Mei 29, 2016 Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi TFF kutangaza maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
  Mei 30, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF kuchapisha orodha ya mwisho ya wagombea na kutangazwa na kubandikwa kwenye mbao za matangazo.
  Mei 31 – Juni 04, Kipindi cha kampeni kwa wagombea.
  Juni 05, 2016 siku ya Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Yanga.
  Wakati huo huo Kamati ya Rufaa ya TFF Jumamosi, itasikiliza pia rufaa ya klabu ya Geita Gold pamoja na rufaa ya kocha msaidizi wa Toto Africans Choke Abeid.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF YAITAKA YANGA KUFANYA UCHAGUZI JUNI 5 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top