• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 22, 2016

  YANGA SC ILIVYOWASILI DAR LEO KUTOKA MISRI

  Wachezaji wa Yanga SC, viungo Haruna Niyonzima (kulia) na Issoufou Boubacar (kushoto) wakijadiliana jambo wakati wanawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam kutoka Cairo, Misri ambako juzi walifungwa mabao 2-1 na Al Ahly katika mechi ya marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya awali kulazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam

  Wazimbabwe wa Yanga ambayo sasa inaangukia kwenye Kombe la Shirikisho, Thabani Kamusoko na Donald Ngoma (nyuma) wakiongozana kutoka JNIA

  Beki wa kulia, Juma Abdul (kulia) na kiungo Said Juma wakitoka ndani ya JNIA

  Kocha Hans van der Pluijm (katikati) wakati wa kuwasili mchana wa leo
  Mashabiki waliojitokeza kuilaki timu wakicheza kwa furaha Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC ILIVYOWASILI DAR LEO KUTOKA MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top