• HABARI MPYA

  Sunday, April 24, 2016

  ZESCO UNITED YAVUNJA MWIKO WA KUTOSHINDA CHOMA

  Shujaa wa Zesco, beki Mkenya, David Owino 
  MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Faz Super League, Zesco United wameshinda mechi ya tatu mfululizo baada ya kuilaza 1-0 ugenini Green Eagles mjini Choma.
  Ushindi huo unamaliza ukame wa ushindi katika mechi za ugenini kwa Zesco dhidi ya Eagles mjini Choma, ambako awali wafungwa mechi mbili na kutoa sare moja kwa zaidi ya misimu mitatu iliyopita.
  Zesco pia walifunga 1-0 na Eagles mwaka 2015 ambao leo wamefungwa kwa mara ya kwanza Choma tangu Septemba mwaka 2012 walipofungwa 2-0 na Zesco.
  Beki wa Kenya, David Owino ndiye aliyefunga bao pekee dakika ya 87 na kuipandisha Zesco nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kutoka ya tisa, wakizidiwa pointi saba na vinara, Nkana wakiwa na mechi tatu pia mkononi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZESCO UNITED YAVUNJA MWIKO WA KUTOSHINDA CHOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top