• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 27, 2016

  HII NDIYO KATIBA ITAKAYOTUMIKA KATIKA UCHAGUZI WA YANGA

  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema kwamba uchaguzi wa Yanga utafanyika chini ya katiba iliyosajiliwa Msajili wa Vyama na Klabu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
  Taarifa ya TFF leo imesema kwa mujibu wa sheria ya BMT ya mwaka 1968 na kama ilivyorekebishwa mwaka 1971, Msajili wa vilabu na vyama vya michezo ndiye mwenye mamlaka ya kusajili katiba za vilabu na za vyama vya michezo.
  "Kwa kuzingatia nguvu za mamalaka haya hivyo uchaguzi ujao wa yanga pamoja na chaguzi zote za vyama wanachama wa TFF zitafanyika kwa kusimamia kwenye Katiba halali iliyosajiliwa na kutambuliwa na Msajili wa vilabu na vyama vya michezo,"imesema taarifa ya TFF.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HII NDIYO KATIBA ITAKAYOTUMIKA KATIKA UCHAGUZI WA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top