• HABARI MPYA

  Sunday, April 24, 2016

  EUROPA LEAGUE YAMUITA NGOMA, WAZUNGU WAFIKA BEI LAKINI YANGA WANABANA

  Na Somoe Ng'itu, TANGA
  TIMU moja ya Ligi Kuu ya Yugoslavia ambayo mwakani itacheza michuano ya Europa League inamtaka mshambuliaji wa Yanga SC, Mzimbabawe Donald Dombo Ngoma.
  Chanzo cha habari kutoka Yanga kimesema kwamba klabu hiyo inataka kufanya mazungumzo na uongozi juu yay a biashara ya Ngoma.
  Chanzo hicho kilisema kwamba katika barua yao ambayo wameituma tena kuwakumbusha Yanga juu ya kumuhitaji Ngoma, wamesema kwamba wako tayari kumnunua kwa dau la Dola za Marekani 350,000 (zaidi ya Sh. milioni 700 za Tanzania).
  Donald Ngoma anatakiwa na klabu itakayocheza Europa League msimu ujao

  "Yule wakala bado anakumbusha barua yake kuhusiana na kumuhitaji Ngoma, lakini Yanga hawataki hata kukaa mezani kuzungumza, na wamesema wako tayari kuongeza dau endapo watatakiwa kufanya hivyo," kilisema chanzo chetu.
  Kiliendelea kusema kwamba straika mwenyewe yuko tayari kwenda kujiunga na timu hiyo na anaitaka Yanga ikubali kufanya mazungumzo.
  Ngoma aliye katika msimu wake wa kwanza katika Mkataba wa miaka miwili aliosaini kutoka FC Platinums ya Zimbabwe Julai mwaka jana, ametokea kuwa kipenzi cha wan Yanga kutokana na shughuli yake uwanjani.
  Katikati ya wiki, Ngoma alifunga bao pekee Yanga ikilala 2-1 mbele ya wenyeji, Al Ahly Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria, Misri katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya awali kulazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam.
  Lakini sasa Yanga itamenyana na Sagrada Esperanca ya Angola kuwania kuingia kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, mechi ya kwanza ikichezwa Dar es Salaam kati ya Mei 6 na 8 na marudiano ugenini kati ya mei 17 na 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: EUROPA LEAGUE YAMUITA NGOMA, WAZUNGU WAFIKA BEI LAKINI YANGA WANABANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top