• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 24, 2016

  YANGA NA COASTAL KATIKA PICHA LEO MKWAKWANI

  Beki wa Coastal Union, Miraj Adam (kushoto) akigeuka na mpira baada ya kumzidi maarifa mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma (kulia) katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Mechi hiyo ilivunjika dakika ya 110 kati ya 120 baada ya mashabiki kumjeruhi mshika kibendera namba mbili, Charles Simon wa Dodoma, Yanga ikiwa inaongoza kwa mabao 2-1
  Beki wa Coastal Union, Hamad Juma akimtoka kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima

  Viungo Mcameroon wa Coastal Union, Youssouf Sabo (kushoto) na Mnyarwanda Haruna Niyonzima wa Yanga kulia wakipambana

  Beki wa Yanga, Oscar Joshua (kushoto) akimtoka kiungo wa Coastal Union, Youssouf Sabo

  Kikosi cha Yanga leo Uwanja wa Mkwakwani kabla ya mchezo huo

  Kikosi cha Coastal Union leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kabla ya mchezo na Yanga

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA NA COASTAL KATIKA PICHA LEO MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top