• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 29, 2016

  BOBAN NA WENGINE WATATU HAWAPO KESHO MBEYA CITY NA MTIBWA MANUNGU

  Na Doreen Favel, MBEYA
  MBEYA City itawakosa wote, Shamte Moshi 'Boban' katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kesho dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu, Turiano Morogoro.
  Kocha Mkuu wa Mbeya City, Kinnah Phiri raia wa Malawi ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kwamba pamoja na Shamte na Boban, katika mchezo huo atawakosa pia Raphael Daud na Themi Felix.

  Phiri, kocha wa zamani wa Free State Stars ya Afrik Kusini amesema Shamte anatumikia adhabu ya kadi za njano, wakatiBoban na Nahodha Temi Felix ambaye kwa muda mrefu wamekuwa nje ya kikosi kutokana na matatizo ya kifamilia.
  Haruna Moshi 'Boban' hatakuwepo kesho Mbeya City ikimenyana na Mtibwa Sugar

  Phiri tayari yupo Manungu na wachezaji 18 aliowateua kwa ajili ya mchezo huo ambao amepania kushinda kutoka ili asogee mbele katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya 10 hadi ya nane angalau.
  “Msimamo wa ligi unaonyesha tuko kwenye nafasi ya 10, hili siyo tatizo sana kwa sababu kushinda mechi mbili zijazo kutatuingiza kwenye timu nane bora, hili ndiyo lengo letu, tunayo michezo minne, mbele nina uhakika kwamba kila mchezaji anafahamu kuwa tunatakiwa kuongeza pointi zaidi ili tumelize ligi tukiwa sehemu ya timu nane za juu” alisema. 
  Baadhi ya wachezaji walio na Mbeya City Manungu ni pamoja na Juma Kaseja, Haningtony Kalyesubhula, John Jerome, John Kabanda, Yusuph Abdalah, Deo Julius, Tumba Lui, Hassan Mwasapili, Kenny Ally, Hamidu Mohamed na Meshack Samuel.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BOBAN NA WENGINE WATATU HAWAPO KESHO MBEYA CITY NA MTIBWA MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top