• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 28, 2016

  FARID MUSSA AFANYIWA VIPIMO VYA MOYO, YUSSUF BAKHRESA AUNGANA NAYE HISPANIA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  BAADA ya kumfanyia majaribio ya siku tatu, klabu ya ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Pili Hispania, ijulikanayo kama Segunda, imemfanyia vipimo vya moyo mchezaji wa kimataifa wa Tanzania, Farid Mussa Malik.
  Winga huyo wa Azam FC amefanyiwa vipimo hivyo Jumatano na Alhamisi majibu yanatarajiwa kutoka na baada ya hapo mustakabli wake zaidi utajulikana.
  Mmoja wa Wajumbe wa bodi ya Ukurugenzi ya Azam FC, Yussuf Bakhresa tayari yuko Tenerife kwa ajili ya kufuatilia kwa karibu majaribio ya mchezaji huyo chipukizi anayeinukia vizuri katika ulimwengu wa soka.
  Farid Mussa (kulia) akiwa na Yussuf Bakhresa nchini Hispania ambako anaendelea na majaribio ya kucheza soka ya kulipwa 

  “Nimefika hapa leo, na nipo na Farid na wakala wake, wanasema mambo yanaendelea vizuri na leo amefanyiwa vipimo vya moyo, kwa hivyo tutajua zaidi kuanzia kesho,”amesema Yussuf Bakhresa akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE usiku wa Jumatano.
  Awali, Farid ilikuwa apelekwe moja ya klabu za Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga, kati ya Las Palmas na Athletic ya Bilbao kwa majaribio, lakini wakala wake akashauri mchezaji huyo aanzie timu ya Daraja la Kwanza Hispania ili kupata nafasi ya kucheza na kuinuka haraka.
  Farid alikwenda Hispania Alhamisi iliyopita akitoka kuichezea klabu yake, Azam FC katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Esperance walioshinda 3-0 mjini Tunis Jumanne.
  Farid alifunga bao la kwanza na kuseti la pili lililofungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’ katika mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam dhidi ya Esperance Azam FC ikitoka nyuma kwa 1-0 na kushinda 2-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FARID MUSSA AFANYIWA VIPIMO VYA MOYO, YUSSUF BAKHRESA AUNGANA NAYE HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top