• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 28, 2016

  FARID MUSSA APAGAWISHA KINOMA HISPANIA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KLABU ya ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Pili Hispania, ijulikanayo kama Segunda inaonekana kuendelea kuridhiwa na uwezo wa mchezaji wa kimataifa wa Tanzania, Farid Mussa Malik (pichani kushoto).
  Tenerife ilimuanzishia kwenye kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 18 Farid ambako amefuzu vizuri mtihani wa kwanza na sasa anapandishwa timu ya wakubwa kwa majaribio zaidi.
  Mmoja wa Wajumbe wa bodi ya Ukurugenzi ya Azam FC, Yussuf Bakhresa ambaye yuko Tenerife kwa ajili ya kufuatilia kwa karibu majaribio ya Farid amesema hadi sasa mambo ni mazuri.
  Farid Mussa (kushoto) akiwa kwenye mazoezi na U-18 ya Tenerife
  Farid Mussa (mbele) akikimbilia mpira kwenye mazoei hayo ambayo imeelezwa amefanya vizuri na sasa anapandishwa timu ya wakubwa 

  “Kwa kweli kijana (Farid) anaendelea vizuri na leo nimehudhuria mazoezi yao, kwa kweli Farid anafanya vizuri na jamaa wanamfurahia sana. Wanamuelekeza sana, fanya hivi na hivi na wamempenda sana,”amesema Yussuf Bakhresa akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo.
  Yussuf amesema kwamba leo Farid anatarajiwa kufanyiwa vipimo vingine vya afya baada ya jana kuchukuliwa vipimo vya moyo. “Nasikia wanataka wamimpime mifupa yake,”amesema Yussuf, ambaye MKurugenzi Mkuu wa Uhai Production, wamiliki wa Azam Media Limited.
  Awali, Farid ilikuwa apelekwe moja ya klabu za Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga, kati ya Las Palmas na Athletic ya Bilbao kwa majaribio, lakini wakala wake akashauri mchezaji huyo aanzie timu ya Daraja la Kwanza Hispania ili kupata nafasi ya kucheza na kuinuka haraka.
  Yussuf Bakhresa (kushoto) akiwa na Farid Mussa baada ya mazoezi na Tenerife leo
  Farid alikwenda Hispania Alhamisi iliyopita akitoka kuichezea klabu yake, Azam FC katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Esperance walioshinda 3-0 mjini Tunis Jumanne.
  Farid alifunga bao la kwanza na kuseti la pili lililofungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’ katika mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam dhidi ya Esperance Azam FC ikitoka nyuma kwa 1-0 na kushinda 2-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FARID MUSSA APAGAWISHA KINOMA HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top