• HABARI MPYA

    Wednesday, April 27, 2016

    SIMBA SC YAMFUNGIA MWEZI MMOJA ABDI BANDA

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC imemfungia kwa mwezi mmoja beki wake, anayeweza kucheza nafasi za kiungo pia, Abdi Banda (pichani kulia).
    Simba imemfungia Banda tangu Aprili 1 na maana yake atakuwa huru kurejea kikosini mwishoni mwa mwezi huu.
    Pamoja na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kuinasa barua ya kufungiwa kwa Banda, lakini bado Siimba imeendelea kufaya siri.
    Ofisa Habari wa Simba, Hajji Sunday Manara alisema suala la Banda litatolewa ufafanuzi  ili mchezaji huyo aweze kujua hatima Jumatano. “Kesho (Jumatano) tunakwenda kutoa uamuzi wa suala la Banda, tumekaa na kujadili utetezi wake, sasa tunatoa hukumu,”alisema Manara.
    Banda alimgomea kocha Mganda, Jackson Mayanja kuingia dakika ya tano katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, kuchukua nafasi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, akidai ni mapema mno kumtoa beki mwenzake kwa sababu ya makosa machache aliyofanya.

    Barua ya Simba SC kumfungia kwa mwezi mmoja Abdi Banda

    Baada ya mchezo huo ambao Simba ilishinda mabao 2-0, uongozi wa Simba alimtaka Banda kumuomba msamaha kocha Mayanja, lakini akagoma na tangu hapo hakuripoti mazoezini.
    Baadaye Banda akatakiwa kuandika barua ya kujieleza kwa nini asichukuliwe hatua kwa utovu wa nidhamu aliofanya, naye akafanya hivyo, ingawa Simba SC wamechukua muda mrefu kutoa uamuzi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAMFUNGIA MWEZI MMOJA ABDI BANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top