• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 27, 2016

  AZAM FC YAIPIGA KUMBO SIMBA MBIO ZA UBINGWA, YAICHAPA 2-0 MAJIMAJI CHAMAZI

  AZAM FC imeipiga kumbo Simba SC katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 2-0 jioni ya leo dhidi ya Majimaji ya SOngea Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Shujaa wa Azam FC leo alikuwa ni kiungo Mudathir Yahya Abbas aliyefunga mabao yote mawili kipindi cha pili, dakika ya 51 na 63.
  Mudathir Yahya (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake wa Azam FC baada ya kufunga leo

  Azam FC sasa pointi 58 baada ya kucheza mechi 25 za Ligi Kuu na kupanda hadi nafasi ya pili, nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga yenye pointi 62 za mechi 25 pia, ikiiteremshia Simba yenye pointi 57 za mechi 25 pia nafasi ya tatu.
  Kikosi cha Azam FC leo kilikuwa; 28 Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael/ Abdallah Kheri dk71, David Mwantika, Aggrey Morris, Jean Mugiraneza, Ramadhan Singano ‘Messi’, Mudathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Didier Kavumbagu/Ame Ali ‘Zungu’ k46 na Khamis Mcha/ Shaaban Iddi dk84.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAIPIGA KUMBO SIMBA MBIO ZA UBINGWA, YAICHAPA 2-0 MAJIMAJI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top