• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 26, 2016

  FARID MUSSA ATUA DEPORTIVO, APEWA MECHI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM 
  WINGA wa Azam FC, Farid Mussa Malik jana amepelekwa klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Pili Hispania (Segunda), ligi ya pili kwa ukubwa Hispania baada ya La Liga.
  Farid alitarajiwa kupewa dakika kadhaa za kucheza mechi usiku wa Jumatatu, kabla ya kuanza majaribio yake rasmi CD Tenerife, inayotumia Uwanja wa Heliodoro Rodriguez Lopez, visiwa vya mjini Tenerife, visiwa vya Canary, Hispania.
  Wakala wa Farid, ameshauri mchezaji huyo aanzie timu ya Daraja la Kwanza Hispania ili kupata nafasi ya kucheza na kuinuka haraka, hiyo ikiwa tofauti na mpango wa awali wakati anamchukua kutoka Azam FC, kwamba angempeleka timu mojawapo ya La Liga kati ya Las Palmas na Athletic ya Bilbao.
  Farid Mussa akiwa makao makuu ya Deportivo Tenerife, Uwanja wa Heliodoro Rodriguez Lopez, visiwa vya mjini Tenerife, visiwa vya Canary, Hispania

  Farid alikwenda Hispania Alhamisi akitoka kuichezea klabu yake, Azam FC katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Esperance walioshinda 3-0 mjini Tunis Jumanne.
  Farid alifunga bao la kwanza na kuseti la pili lililofungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’ katika mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam dhidi ya Esperance Azam FC ikitoka nyuma kwa 1-0 na kushinda 2-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FARID MUSSA ATUA DEPORTIVO, APEWA MECHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top