• HABARI MPYA

    Sunday, July 05, 2015

    TEFA YAPATA OFISA HABARI

    CHAMA cha Soka Temeke (TEFA) kimemteua Mwandishi wa Habari za michezo, Ben Mwanantala kuwa Ofisa Habari wa chama hicho.    
    Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Dar es Salaam, Katibu wa TEFA, Kassim Mustapha amesema kwamba wamemteua Mwanantala kutokana na mchango wake mkubwa katika chama hicho, ikiwemo utoaji wa habari na matukio mbalimbali ya michezo Temeke.
    Mbali na hilo pia, Kamati ya uchaguzi ya TEFA, imetaja tarehe ya kufanyika uchaguzi wa chama hicho ambayo ni Agosti 16, 2015
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TEFA YAPATA OFISA HABARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top