• HABARI MPYA

    Sunday, July 19, 2015

    MESSI, BALOU NA WANGA WATEMWA AZAM FC KIKOSI CHA KAGAME

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall hajawajumuisha kiungo Kipre Michael Balou, winga Ramadhani Singano ‘Messi’ na mshambuliaji Alan Wanga katika kikosi chake cha wachezaji 20 watakaocheza Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
    Hall hajawajumuisha wachezaji hao, Messi aliyesajiliwa kutoka Simba SC kama mchezeji huru, Balou raia wa Ivory Coast na Mkenya Wanga anayewania kusajiliwa kutoka El Merreikh ya Sudan kwa sababu tofauti.
    Messi hataonekana kwenye Kombe la Kagame 2015 Azam FC 

    Balou na Messi wote hawako fiti kwa asilimia 100, wakati Wanga mazungumzo kwa ajili ya kusajiliwa kwake yanaendelea.
    Kikosi cha Azam FC kwa ajili ya Kagame kinaundwa na makipa watatu; Manula Aishi Salum, Mwadini Ali na Metacha Boniphance Mnata. 
    Mabeki; Pascal Wawa, Agrey Morris Ambros, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Morad Said Hussein, Kamagi Gadiel Michael na Kheri Abdallah Salum.
    Viungo; ni Mkami Hamid Mao, Salum Abubakar
    Domayo Frank Raymond, Jean Mugiraneza, Abbas Mudathir Yahya na Shah Faridi Mussa na washambuliaji ni Nahodha John Bocco, Didier Kavumbagu, Kipre Tchetche na Ame Ali.
    Azam FC inafungua dimba na KCCA ya Uganda jioni hii mchezo wa Kundi C Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MESSI, BALOU NA WANGA WATEMWA AZAM FC KIKOSI CHA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top