• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 26, 2015

  NGASSA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO FREE STATE, AFUNGA NA KUWASETIA WENGINE ZIARA YA LESOTHO

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa jana amefunga bao lake la kwanza katika timu yake mpya, Free State Stars ya Afrika Kusini ikishinda 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji, Bantu FC Uwanja Leshoboro Seeiso Sports Complex mjini Mafeteng, Lesotho.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE kutoka Mafeting, ambako timu yake imekwenda kucheza mechi za kujiandaa na msimu mpya, Ngassa amesema kwamba ametoa pasi ya bao moja na kufunga katika ushindi wa jana.
  “Leo pia tumecheza mechi na timu nyingine inaitwa Matlaba, tumeshinda 4-0 nimetoa pasi za mabao mawili. Sasa tunajiandaa kurudi Bethelehm kuendelea na maandalizi ya mwishoni kabla ya Ligi,”amesema.
  Ngassa amejiunga na FS ya Bethlehem, Afrika Kusini Mei mwaka huu kama mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake Yanga SC ya Dar es Salaam.
  Huu ni mwanzo mzuri kwa kiungo huyo mshambuliaji wa zamani wa Toto Africans, Kagera Sugar, Azam FC na Simba SC katika timu hiyo inayofundishwa na Mmalawi, Kinnah Phiri. 
  Mrisho Ngassa amefungua akaunti ya mabao Free State Stars

  Mrisho Ngassa tayari ni mchezaji wa kikosi cha kwanza cha Free State
  Tayari ratiba ya Ligi Kuu ya ABSA imetoka na FS itafungua dimba na Black Aces kabla ya kukutana na mabingwa watetezi, Kaizer Chiefs katika mchezo wa pili. Kaizer wataanza kutetea taji lao dhidi ya Chippa United Agosti 8.
  Kwa mujibu wa ratiba ya msimu wa PSL wa 2015-16, Mamelodi Sundowns wataanza na Platinum Stars, Orlando Pirates na SuperSport United, wakati timu mbili zilizopanda msimu huu, Golden Arrows na Jomo Cosmos watakuwa nyumbani na University ya Pretoria na ugenini na Maritzburg United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGASSA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO FREE STATE, AFUNGA NA KUWASETIA WENGINE ZIARA YA LESOTHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top