• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 31, 2015

  MAYUNGA KUACHIA VIDEO YA "NICE COUPLE" CHANELI YA TRACE LEO

  MSHINDI wa shindano la Airtel Trace Music Star Nalimi Mayunga ameachia kibao chake kipya cha " Nice Couple" video itakayorushwa kuanzia leo katika kituo cha DSTV chanel ya Trace Urban 325.
  Mwanzoni mwa mwezi huu. Mshindi huyo wa Airtel Trace Music star alitua mjini Johannesburg South Afrika akitokea nchini Tanzania  ili kuanza safari yake kujiendeleza kimuziki na kufikia ndoto zake mara baada ya kuibuka mshindi wa mashindano makubwa yaliyoshirikisha nchi 13 barani
  Afrika  yaliyofanyika tarehe 18 April 2015.
  Mayunga alitangazwa mshindi na mwanamuziki wa kimataifa wa miondoko ya R& B wa nchini Marekeni, Akon na kupata zawadi nono ikiwemo deli ya kurekodi single ambapo mayunga alishuka nchini South Afrika na kuredoki nyimbo yake ya "Nice Couple" katika maeneo ya Orlando East.
  Nyimbo hii tayari imeshaanza kupigwa katika vyombo na sehemu mbalimbali nchini South Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAYUNGA KUACHIA VIDEO YA "NICE COUPLE" CHANELI YA TRACE LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top