• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 22, 2015

  MASHABIKI WA EINTRACHT FRANKFURT WAWAPA KICHAPO CHA HATARI MASHABIKI WA LEEDS

  MASHABIKI wa Leeds United wamepewa mkong'oto na mashabiki wa Eintracht Frankfurt usiku wa jana baada ya mchezo wa kirafiki baina ya timu hizo  uliofanyika Austria.
  Polisi mjini humo wamewashutumu mashabiki wa timu ya Ujerumani kwa kuanzisha vurugu, ambazo zilisababisha watu 25 wakamatwe na wengine kibao kuachwa wanavuja damu kwa majeraha.
  Taarifa kutoka katika eneo la tukio, zinasema kwamba kundi la mashabiki 100 wa Frankfurt baadhi yao wakiwa wamevaa vitu vya kuficha sura zao, liliwavamia kundi la mashabiki wa Leeds uwanjani baada ya Wajerumani kushinda 2-1. 
  Shabiki wa Eintracht Frankfurt akiruka kumpiga teke la Karate shabiki wa Leeds United baada ya mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mjini Eugendorf, Austria. PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Mara tu baada ya mechi mashabiki wa timu hizo walianza kutupiana makonde na mateke uwanjani mjini Eugendorf, karibu na Salzburg.
  Mashabiki watatu wa Leeds, Maofisa wawili wa Polisi na walinzi wa uwanjani walipelekwa hospitali kwa matibabu. Inaaminika kwamba 17 kati ya waliokamatwa walikuwa mashabiki wa Frankfurt.
  Polisi ilitumia mabomu na mbwa kuwatawanya mashabiki hao waliokuwa katikati ya mpambano mkali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MASHABIKI WA EINTRACHT FRANKFURT WAWAPA KICHAPO CHA HATARI MASHABIKI WA LEEDS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top