• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 26, 2015

  SIMBA SC KUCHEZA MECHI YA KWANZA CHINI YA KERR KESHO

  SIMBA SC kesho inatarajiwa kucheza mchezo wa kwanza chini ya kocha mpya, Muingereza Dylan Kerr itakapomenyana na Kombaini ya Zanzibar Uwanja wa Amaan, visiwani humo.
  Wachezaji wa Simba leo wamepewa mapumziko ya siku moja kwa ajili ya kuupumzisha miili kabla ya kesho Saa 2:00 asubuhi kufanya mazoezi ya viungo tayari kwa kuikabili timu ya Zanzibar Saa 11:00 jioni.
  Kocha Mkuu wa Simba SC, Dylan Kerr amesema mechi ya kesho itakuwa ni kipimo kizuri kwa timu yake kujitayarisha na mechi dhidi ya AFC Leopards ya Kenya katika kilele cha tamasha la Simba Day. 
  "Tunategemea kufanya vizuri katika mchezo wa kesho na si kesho tu bali hata kwenye mechi yetu kubwa ya kwanza na AFC Leopards,”amesema Muingereza huyo.
  Simba itaikabili AFC Leopards Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Siku hiyo, wanachama wote wa Simba wenye kadi mpya wataingia bure uwanjani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUCHEZA MECHI YA KWANZA CHINI YA KERR KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top