• HABARI MPYA

  Thursday, July 23, 2015

  BENTEKE: NIMEKUJA KUSHINDA MATAJI LIVERPOOL

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ubelgiji, Christian Benteke amesema kwamba ametua Liverpool kutoka Aston Villa ili kushinda mataji.
  Benteke, aliyejiunga na timu ya Midlands mwaka 2012 na kuifungia mabao 42 katika mechi 88 za ligi, arrived aliwasili viwanja vya mazoezi vya Wekundu hao, Melwood Jumatano baada ya Liverpool kukamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 32.5.
  Liverpool pia imewasajili washambuliaji Danny Ings kutoka Burnley, na Roberto Firmino kutoka Hoffenheim, ili kuirejeshea makali safu yao ya ushambuliaji inayomkosa wa muda mrefu, Daniel Sturridge na Luis Suarez aliyehamia Barcelona msimu uliopita na Raheem Sterling aliyetimkia Manchester City. 

  Christian Benteke amekamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 32.5 kwenda Liverpool kutoka Aston Villa Jumatano PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  WAPYA WALIOSAJILIWA LIVERPOOL 2015

  Christian Benteke - Pauni Milioni 32.5 kutoka Aston Villa
  Roberto Firmino - Pauni Milioni 29 kutoka Hoffenheim
  Nathaniel Clyne - Pauni Milioni 12.5 kutoka Southampton
  Joe Gomez - Pauni Milioni 3.5 kutoka Charlton
  Danny Ings kutoka Burnley
  James Milner kutoka Manchester City
  Adam Bogdan kutoka Bolton
  JUMLA IMETUMIA: 
  Pauni Milioni 77.5 
  Akizungumza mara baada ya kukamilisha uhamisho wake, Benteke alisema; "NIna furaha sana kuwa hapa na ningependa kumshukuru mmiliki, Ian (Ayre) na pia kocha kwa jitihada zao za kunifikisha hapa.
  "Nafikiri ilikuwa klabu sahihi, kwa sababu nilikuwa nina mawasiliano mazuri na kocha na nilitaka kuwa sehemu ya mipango yake. 
  "Nafahamu Liverpool ni habari kubwa. Wameshinda mataji mengi ya Ligi Kuu na matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na pia Kombe la UEFA na mataji mengi. Nafahamu ni klabu kubwa.
  Alipoulizwa ni kipi kinamhamasisha yeye kama mchezaji, alisema: "Ni juu ya kushinda mataji. Ni kuhusu kufanya kitu fulani katika kazi yangu ambacho naweza labda kuwaeleza wanangu nilichokifanya,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BENTEKE: NIMEKUJA KUSHINDA MATAJI LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top