• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 24, 2015

  MSUVA HAYUMO KABISA KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA KMKM, TAMBWE AANZISHIWA BENCHI

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MFUNGAJI bora  na mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simon Msuva hayumo kabisa katika kikosi cha Yanga SC kinachocheza leo dhidi ya KMKM Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mchezaji 
  Mchezaji aliyemfuatia Msuva kwa mabao Yanga SC msimu uliopita, Mrundi Amissi Tambwe yeye ameanzishiwa benchi kuelekea mchezo huo wa Kundi A Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame unaonza Saa 10:00 jioni.
  Wawili hao wote walikosa penalti, Yanga SC ikishinda 3-0 dhidi ya Telecom ya Djibouti juzi Uwanja wa Taifa na ni Msuva aliyesababisha matuta yote hayo. 
  Simon Msuva aliumia katika mechi dhidi ya Telecom

  Msuva hayumo kabisa kikosini kwa sababu anaumwa goti baada ya kuumia katika mechi dhidi ya Telecom. 
  Makocha wa Yanga SC, Mholanzi, Hans van der Pluijm na Charles Boniface Mkwasa wamewaanzisha wachezaji wapya watupu katika safu ya ushambuliaji leo, Godfrey Mwashiuya, Deus Kaseke, Malimi Busungu na Mzimbabwe Donald Ngoma.
  Kwa ujumla kikosi cha Yanga SC langoni atasimama Ally Mustafa ‘Barthez’, beki ya kulia Juma Abdul, kushoto Mwinyi Hajji Mngwali na katikati Kevin Yondan na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, wakati viungo ni Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima.
  Wachezaji wa akiba ni Deo Munishi ‘Dida’, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Andrey Coutinho, Amissi Tambwe, Kpah Sherman na Joseph Zutah.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSUVA HAYUMO KABISA KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA KMKM, TAMBWE AANZISHIWA BENCHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top