• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 27, 2015

  TP MAZEMKBE YAFUFUA MATUMAINI LIGI YA MABINGWA AFRIKA, EL MERREIKH NAYO…

  TP Mazembe ya DRC imefufua matumaini ya kutwaa ubingwa wa Afrika msimu baada ya kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili mzunguko wa kwanza hatua ya makundi ya Ligi Mabingwa Afrika.
  Mazembe iliyoanza vibaya kwa sare mbili mfululizo nyumbani na ugenini, mwishoni mwa wiki ilipata ushindi wa ugenini wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Smouha ya Misri.
  Na sasa Mazembe yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanafikisha pointi tano sawa na El Hilal ya Sudan inayoongoza Kundi A kwa wastani mzuri wa mabao.
  Hilal ilipunguzwa kasi jana baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Moghreb Tetouan nchini Morocco. Smouha inayocheza michuano ya Afrika kwa mara ya kwanza kabisa mwaka huu, inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake tatu, wakati Moghreb Tetouan wanaburuza mkia kwa pointi zao mbili.
  Mechi za Kundi B zilizochezwa mwishoni mwa wiki, ES Setif ya Algeria ililazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na El Merreikh ya Sudan, wakati USM Alger iliichapa 2-1 MC Eulma, zote za Algeria.
  USM Alger inaongoza Kundi B baada ya kushinda mechi zake zote tatu na kujikusanyia pointi tisa, wakifuatiwa na El Merreikh wenye pointi nne sawa na ES Setif, wakati MC Eulma hawana pointi.
  Mechi za mzunguko wa pili zitaanza Agosti 8, mwaka huu, TP Mazembe wakiwakaribisha Smouha, MC Eulma na USM Alger wakionyeshana kazi Algeria, El Hilal wakiwa wenyeji wa Moghreb Tetouan na El Merreikh wakiwakaribisha ES Setif.
  TP Mazembe wakifuarahia ushindi wao wa kwanza Ijumaa nchini Misri

  MISIMAMO YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

  Kundi A


  PWDLGFGAGDPts
  1Al Hilal (Sudan)31203125
  2TP Mazembe (DRC)31202025
  3Smouha (Misri)310236-33
  4Moghreb Tetouan (Morocco)302134-12

  Kundi B  PWDLGFGAGDPts
  1USM Alger (Algeria)33005239
  2Al Merreikh (Sudan)31113214
  3ES Setif (Algeria)31113304
  4MC Eulma (Algeria)300315-40
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TP MAZEMKBE YAFUFUA MATUMAINI LIGI YA MABINGWA AFRIKA, EL MERREIKH NAYO… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top