• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 29, 2015

  KCCA YATINGA NUSU FAINALI KAGAME, SASA YASUBIRI MSHINDI KATI YA AZAM FC NA YANGA

  Wachezaji wa KCCA FC wakisherehekea ushindi wao leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  KCCA ya Uganda imetinga Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuichapa mabao 3-0 Al Shandy ya Sudan mchana wa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  KCCA inayofundishwa na Mike Muteebi, sasa inaungana na Gor Mahia ya Kenya ana Khartoum N ya Sudan zilizotinga Nusu Fainali jana. Gor Mahia iliifunga 2-1 Malakia ya Sudan Kusini wakati Khartoum iliichapa 4-0 APR ya Rwanda.   
  Mabao ya KCCA leo yamefungwa na Joseph Ochaya, Farooque Motovu na Thom Masiko na sasa watasubiri mshindi kati ya Azam FC na Yanga SC zote za Dar es Salaam wanaomenyana jioni hii wakutane naye katika Nusu Fainali Ijumaa. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KCCA YATINGA NUSU FAINALI KAGAME, SASA YASUBIRI MSHINDI KATI YA AZAM FC NA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top