• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 25, 2015

  SHERMAN ANAKWENDA MPUMALANGA BLACK ACES KUFANYA VIPIMO VYA AFYA

  MSHAMBULIAJI Mliberia wa Yanga SC, Kpah Sean Sherman (pichani) anatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Jumatatu kwenda Johannesburg, Afrika Kusini kufanya vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na klabu ya Mpumalanga Black Aces ya Ligi Kuu ya nchi hiyo.
  Sherman aliyejiunga na Yanga SC Desemba mwaka jana, amepata nafasi ya kujiunga na timu hiyo na klabu yake imeridhia aende, baada ya kuleta mshambuliaji mpya, Donald Ngoma kutoka Zimbabwe. 
  Sherman aliyetokea klabu ya Ligi Kuu ya Cyprus Kaskazini, Cetinkaya FC, ambayo alikuwa anaichezea kwa mkopo kutoka Aries FC ya kwao Liberia hadi sasa ameichezea Yanga SC mechi 27 na kuifungia mabao sita tu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SHERMAN ANAKWENDA MPUMALANGA BLACK ACES KUFANYA VIPIMO VYA AFYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top