• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 20, 2015

  BLATTER APATA AIBU YA KUONDOKEA FIFA, AMWAGIWA DOLA FEKI ZA 'HONGO' HADHARANI

  RAIS wa FIFA, Sepp Blatter leo amemwagiwa maburungutu ya dola feki na mchekeshaji, Muingereza Simon Brodkin aliyevamia Mkutano wake na Waandishi wa Habari mjini Zurich, Uswisi.
  Brodkin ambaye pia anafahamika kama Jason Bent na Lee Nelson alikwenda kwenye meza ya Blatter mbele ya jukwaa na kumuonyesha dola feki akisema; "Hizi ni kwa ajili ya Korea Kaskazini 2026,".
  Baadaye akawageukia Waandishi wa Habari wakati Blatter, ambaye alitangaza hatagombea Urais wa FIFA katika uchaguzi ujao baada ya kujiuzulu mapema mwaka huu, aliwaita walinzi haraka waje kumuondoa 'kituko huyo'.
  Walinzi walimfikia haraka Brodkin, lakini kabla hawajamtoa akamwagia maburungutu ya dola hizo feki Blatter ambazo zilikuwa zinapeperuka juu kumzunguka rais huyo wa soka duniani.  
  Noti feki za dola zikipeperuka kumzunguka Rais wa FIFA, Sepp Blatter baada ya kumwagiwa na mchekeshaji Simon Brodkin leo makao makuu ya bodi hiyo ya soka duniani mjini Zurich, Uswisi PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Mwaka jana alivamia jukwaa la Stereo Kicks’ X-Factor akiigiza kuungana na wachezaji wa England kwenye ndege kwa safari ya Kombe la Dunia Brazil. Mapema mwaka huu, alimshangaza rapa Kanye West huko Glastonbury kwa kumuibukia jukwaani bila kuitwa. 
  Blatter alikuwa anazungumzia tarehe ya uchaguzi mpya wa FIFA kujaza nafasi yake, ambao amesema utafanyika Februari 26, mwakani. Simon Brodkin alichukuliwa kwenye gari la Polisi wa Uswisi walioondoka naye kutoka mabao makuu hayo ya FIFA.
  FIFA inakabiliwa tuhuma nzito za rushwa na inadaiwa hata uenyeji wa Kombe la Dunia hutolewa baada ya hongo. Tuhuma ambazo zilitolewa ushahidi ni za uenyeji wa Kombe la mwaka 2010 Afrika Kusini kwamba nchi hiyo ilihonga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BLATTER APATA AIBU YA KUONDOKEA FIFA, AMWAGIWA DOLA FEKI ZA 'HONGO' HADHARANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top