• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 31, 2015

  GOR MAHIA YATANGULIA FAINALI KOMBE LA KAGAME, YAWAPIGA WASUDAN 3-1 TAIFA

  Mashabiki wa Gor Mahia wakifurahia leo Uwanja wa Taifa wakati timu yao ikiiadhibu Khartoum
  GOR Mahia ya Kenya imetinga ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Khartoum N ya Sudan mchana wa leo.
  Kwa ushindi huo katika mchezo wa Nusu Fainali uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Gor Mahia sasa watasubiri mshindi kati ya Azam FC ya Tanzania na KCCA ya Uganda wakutane katika fainali Jumapili.
  Mabao ya Gor Mahia leo yamefungwa na Michael Olunga kwa penalti, Innocent Wafula na Meddie Kagerem, wakati bao pekee la Khartoum limefungwa na Amin Ibrahim Elman, 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GOR MAHIA YATANGULIA FAINALI KOMBE LA KAGAME, YAWAPIGA WASUDAN 3-1 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top