• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 23, 2015

  APR WAENDELEZA MAANGAMIZI KOMBE LA KAGAME, WAWAPIGA WARUNDI 2-1 TAIFA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  APR ya Rwanda imejihakikishia kwenda Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya LLB AFC ya Burundi jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
  Timu hiyo ya Jeshi la Rwanda sasa inafikisha pointi tisa, baada ya kushinda mechi zake zote tatu na kupaa kileleni kabisa mwa Kundi B, ikifuatiwa na Al Shandy ya Sudan yenye pointi nne, LLB pointi mbili na Heegan ya Somalia pointi moja baada ya kila timu kucheza mechi tatu.
  APR ililazimika kutoka nyuma katika mchezo wa leo ili kupata ushindi huo, kwani Nahimana Abdul alianza kuifungia LLB dakika ya 48 baada ya kuwatoka mabeki wa timu ya Rwanda.
  Lakini Sibomana Patrick aliisawazishia APR dakika ya 57 kwa penalti iliyotolewa na refa wa Tanzania, Martin Saanya kufuatia beki wa LLB kuunawa mpira kwenye boksi.
  Issa Bigirimana akaunganisha vizuri krosi ya Fiston Nkizingabo kuifungia APR bao la ushindi dakika ya 89. Katika mchezo uliotangulia, Al Shandy ya Sudan iliifunga mabao 3-2 Heegan ya Somalia. 
  Kikosi cha APR kilikuwa; Ndoli Claude, Rusheshangoga Michael, Mubumbyi Barnabe/Ruhinda Faruk dk46, Rutanga Eric, Nsabimana Erick/Mukunzi Yannick dk71, Rugwiro Herve, Bigirimana Issa, Rwatubyaye Abdoul, Simbomana Patrick, Sekamana Maxime/Nkinzingabo Fiston dk74 na Buteera Andrew. 
  LLB AFC; Mbonihankuye Innocent, Hakizi Mana Issa, Manirakiza Aruna,Kiza Fataki, Uwimana Messo, Duhayindavyi Gael, Nshimiri Mana Abassi, Ndaye  Chancel, Niyonkuru Pascal/Iddy Said dk49, Ndarusanze Jean Claude na Murutabose Emedy/ Nahimana Abdoul dk48. 
  Nyota wa APR, Simbomana Patrick akipasua katikati ya wachezaji wa LLB katika mchezo wa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  MISIMAMO YA MAKUNDI KOMBE LA KAGAME 2015

  Kundi A

  TIMUPWDLGDPTS
  1Khartoum220066
  2Gor Mahia220036
  3Young Africans FC210123
  4KMKM3102-23
  5Telecom3003-90
  Kundi B

  TIMUPWDLGDPts
  1APR330049
  2AlShandy311104
  3LLB AFC3021-12
  4Heegan3012-31
  Kundi C

  TimuPWDLGDPTS
  1Azam FC220036
  2KCC FC210103
  3Malakia2101-13
  4Adama City2002-20
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: APR WAENDELEZA MAANGAMIZI KOMBE LA KAGAME, WAWAPIGA WARUNDI 2-1 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top