• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 31, 2015

  VILLA YASAJILI MIDO HATARI LA UFARANSA, WAPYA SASA WAFIKA NANE

  KLABU ya Aston Villa imemsajili kiungo Mfaransa, Jordan Veretout mwenye umri wa miaka 22, aliyesaini Mkataba wa mitano kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 8 kutoka Nantes ya kwao.
  Veretout, mchezaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Ufaransa, alikuwa pia anawaniwa na Leicester City lakini akachagua kwenda kuendeleza kipaji chake Villa Park ambako ametambulishwa rasmi leo akiwa mchezaji wa nane kusajiliwa na kocha Tim Sherwood.
  Wengine ni washambuliaji Rudy GestedeEmmanuel Adebayor, Micah Richards, Mark Bunn, Idrissa Gueye, Jordan Amavi, Jordan Ayew na Jose Angel Crespo waliosajiliwa baada ya kuuzwa kwa bei nzuri Fabian Delph na Christian Benteke.
  Aston Villa imemtambulisha kiungo Mfaransa, Jordan Veretout mwenye umri wa miaka 22 aliyesaini Mkataba wa miaka mitano PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VILLA YASAJILI MIDO HATARI LA UFARANSA, WAPYA SASA WAFIKA NANE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top