• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 31, 2015

  SIMBA SC YA DYLAN KERR WEKA MBALI NA WANYONGE, YAUA 4-0 ZENJI

  Kikosi cha Simba SC kilichoanza jana Zanzibar
  KOCHA mpya wa Simba SC, Muingereza Dylan Kerr jana ameiongoza timu hiyo kushinda mechi ya pili tangu aanze kazi mwezi uliopita baada ya kuichaoa Black Sailor mabao 4-0 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Mabao ya Simba Sc jana yamefungwa na 4-0 Abdi Banda dakika ya nne, Ibrahim Hajib dakika ya 24, Elias Maguri dakika ya 80 na Boniphace Magesa dakika ya 89.
  Huo ni mchezo wa pili wa kirafiki katika kambi ya kujiandaa na msimu Tanga Simba inashinda chini ya Kerr, baada ya awali kushinda 2-1 dhidi ya Kombaini ya Zanzibar, mabao yake yakifungwa na Mussa Mgosi na Hamisi Kiiza.
  Kocha Kerr kushoto na benchi nzima la Ufundi jana Uwanja wa Amaan 
  Mshambuliaji wa Simba SC, Hamisi Kiiza akitafuta maarifa ya kumtoka beki wa Black Sailor jana


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YA DYLAN KERR WEKA MBALI NA WANYONGE, YAUA 4-0 ZENJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top