• HABARI MPYA

    Monday, July 27, 2015

    AL AHLY NA ZAMALEK ZANG’ARA AFRIKA, ZOTE ZAONGOZA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO

    VIGOGO wa Misri, Al Ahly na Zamalek wote wamemaliza kileleni mwa makundi baada ya mzunguko wa kwanza Kombe la Shirikisho Afrika mwishoni mwa wiki.
    Ushindi wa 2-0 jana wa Zamalek nyumbani dhidi ya AC Leopards Kongo, umewafanya waongoze Kundi B kwa kufikisha pointi tisa, wakati Ahly baada ya kuifunga  1-0 Etoile du Sahel ya Tunisia juzi mjini Alexandria sasa wanaongoza Kundi A kwa kufikisha pointi saba.
    Mechi nyingine za mwishoni mwa wiki, CS Sfaxien ya Tunisia ilifungwa 1-0 nyumbani na Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Esperance ya Tunisia ilifungwa pia nyumbani 2-1 na Stade Malien ya Mali.
    Al Ahly ina pointi saba kileleni mwa Kundi A, ikifuatiwa na ES Sahel yenye pointi sita, Stade Malien pointi nne na Esperance ambayo haina pointi inaburuza mkia.
    Zamalek ina ponti tisa kileleni mwa Kundi B, ikifuatiwa na Orlando Pirates pointi sita CS Sfaxien pointi nne na AC Leopards pointi moja.

    Mechi za mzunguko wa pili Kombe la Shirikisho zitaanza Agosti 8 mwaka huu, Orlando Pirates wakiikaribisha CS Sfaxien, AC Leopards wakiwakaribisha Zamalek, Stade Malien wakiwa wenyeji wa Esperance na ES Sahel wakiwakaribisha Al Ahly.
    Al Ahly wanaongoza Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika

    MISIMAMO YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

    Kundi A



    PWDLGFGAGDPts
    1Al Ahly (Misri)32104047
    2ES Sahel (Tunisia)32012116
    3Stade Malien (Mali)31112204
    4Esperance (Tunisia)300316-50

    Kundi B



    PWDLGFGAGDPts
    1Zamalek (Misri)33005149
    2Orlando Pirates32013216
    3CS Sfaxien (Tunisia)301213-21
    4AC Leopards (Kongo)301214-31

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AL AHLY NA ZAMALEK ZANG’ARA AFRIKA, ZOTE ZAONGOZA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top