• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 28, 2015

  KOCHA ALIYEIPA MEXICO UBINGWA WA AMERIKA AFUKUZWA BAADA YA KUMSHAMBULIA MWANDISHI

  KOCHA wa Mexico, Miguel Herrera (pichani kushoto) amefukuzwa leo kwa tuhuma za kumshambulia Mwandishi wa Habari wa Televisheni, siku mbili baada ya kuipa timu hiyo ubingwa wa Gold Cup nchini Marekani.
  Mwalimu huyo 'mtata' mwenye umri wa miaka 47 ambaye aliiongoza timu hiyo kufika hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia ambako ilitolewa na Uholanzi kwa mikwaju ya penalti mwaka jana -- anatuhumiwa kumshambulia mwandishi wa Habari aliyemkosoa, tukio ambalo anadaiwa kufanya Uwanja wa Ndege wa Philadelphia saa kadhaa baada ya Mexico kuifunga Jamaica.
  Herrera, ambaye hajazungumzia chochote juu ya uamuzi huo, amesema alimsukuma 'kiulaini' tu Christian Martinoli aliyekuwa anamuuliza swali. Hata hivyo kitendo hicho kilishuhudiwa na macho ya watu, jambo ambalo limefanya Shirikisho la Soka likose hatua nyingine ya kuchukua zaidi ya kumfukuza.
  "Tumechukua uamuzi wa kumuondoa kocha wa timu ya taifa, Miguel Herrera katika majukumu yake,"amesema Rais wa Shirikisho, Decio de Maria. "Thamani yetu na tarativu zetu lazima zizingatiwe pamoja na matokeo,".
  De Maria hakumtaja mwalimu atakayemrithi Herrera. "Kumfukuza Herrera yalikuwa maamuzi magumu,"amesema De Maria.
  Herrera, beki 'asiye na maana' wa zamani aliyepewa jina la utani 'The Louse', amekuwa kazini timu ya taifa ya Mexico tangu Oktoba mwaka 2013 alipoichukua timu ikiwa inasuasua hadi kuiwezesha kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2014 Brazil.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA ALIYEIPA MEXICO UBINGWA WA AMERIKA AFUKUZWA BAADA YA KUMSHAMBULIA MWANDISHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top