• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 27, 2015

  BOBBY KRISTINA AFARIKI DUNIA AKIWA ANA UMRI WA MIAKA 22

  BOBBI Kristina Brown - mtoto pekee wa mwimbaji nyota wa Marekani Whitney Houston amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 22 baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi sita. 
  Familia yake imesema: "Bobbi Kristina (pichani juu) amefariki dunia Julai 26, 2015 akiwa amezungukwa na familia yake. Hatimaye amepumzika kwa amani kwenye mikono ya Mungu. "Kwa mara nyingine tena tungependa kuwashukuru nyote kwa upendo na mshikamano wenu katika kipindi chote cha kuugua kwake".

  Mama na bintiye: Binti wa miaka 22 amefariki dunia Peachtree Christian Hospice mjini Georgia Jumapili- miaka mitatu tangu kifo cha mama yake, mwimbaji Whitney Houston aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48 mjini Beverly Hills, California. PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BOBBY KRISTINA AFARIKI DUNIA AKIWA ANA UMRI WA MIAKA 22 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top