• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 24, 2015

  YANGA SC YATINGA ROBO FAINALI KAGAME, YAITWANGA KMKM 2-0 TAIFA, MALIMI BUSUNGU ACHANA NAYE…

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imekata tiketi ya kutinga Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMKM ya Zanzibar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo wa Kundi A, mabao yote ya Yanga SC yalipatikana kipindi cha pili, yakifungwa na Malimi Busungu na Amisi Tambwe.
  Busungu alianza kufunga bao la kwanza dakika ya 55 akimalizia pasi ya Mzimbabwe, Donald Ngoma aliyeitoa huku amebanwa na mabeki wa KMKM waliomuwekea ulinzi mkali leo.
  Amisi Tambwe amefunga bao lake la kwanza katika Kagame ya mwaka huu na la pili kwa Yanga SC leo

  Hilo linakuwa bao la tatu kwa Busungu katika mashindano haya na sasa analingana na Michale Olunga wa Gor Mahia na Salah Eldin Osman Bilal  wa Khartoum N.
  Baada hilo liliamsha hamasa ya wachezaji wa Yanga SC ambao kipindi cha kwanza walipoteza nafasi nyingi za wazi.
  Tambwe aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Busungu, aliifungia bao la pili Yanga SC kwa kichwa dakika ya 72 baada ya kuuparaza mpira wa juu uliotokana na krosi ya Ngoma na kumpita kipa wa KMKM, Nassor Abdallah aliyetoka langoni bila hesabu.
  Awali ya hapo, Tambwe alikosa bao la wazi akiwa amebaki yeye na kipa huyo wa KMKM dakika ya 66 baada ya pasi ya Deus Kaseke.
  Mfungaji wa bao la kwanza la Yanga SC, Malimi Busungu (kushoto) akimtoka beki wa KMKM, Khamis Ali Kamis
  Mpishi wa mabao yote ya Yanga SC leo, Donald Ngoma (kushoto) akimtoka beki wa KMKM, Said Idrissa Said
  Malimi Busungu akiruka juu kupiga kichwa, lakini bahati mbaya mpira ulitoka nje
  Winga wa Yanga SC, Deus Kaseke akiwa chini baada ya kukwatuliwa na beki wa KMKM, Ibrahim Khamis Khatib 
  Kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyoonzima (kushoto) akitafuta maarifa ya kumpita kiungo wa KMKM, Mussa Said Athumani

  Kwa matokeo hayo, Yanga SC wanafikisha pointi sita na kujihakikishia kwenda Robo Fainali wakiwa wanashika nafasi ya tatu nyuma ya Knartoum N ya Sudan wanaoongoza kwa pointi zao saba sawa na Gor Mahia ya Kenya.
  Mchezo wa kwanza, Gor Mahia na Kharotum N ziligawana pointi baada ya sare ya 1-1. 
  Mechi za mwisho za Kundi A zitachezwa Jumapili, Yanga ikimaliza na Khartoum N na Gor Mahia ikicheza na Telecom. KMKM imemaliza mechi zake na pointi tatu zilizotokana na ushindi wa 1-0 dhidi ya vibonde Telecom ya Djibouti. 
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul/Joseph Zutah dk83, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite/Andrey Coutinho dk88, Deus Kaseke, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Malimi Busungu/Amisi Tambwe dk60 na Godfrey Mwashiuya.
  KMKM; Kmkm: Nassor Abdullah, Khamis Ali, Tizzo Chomba, Pandu Haji, Said Idrissa, Mussa Said, Mateo Antony, Juma Mbwana, Haji Simba/Maulid Ibrahim dk46, Ibrahim Khamis/Ame Khamis dk46 na Nassor Ali/Fakhi Mwalimu dk68.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YATINGA ROBO FAINALI KAGAME, YAITWANGA KMKM 2-0 TAIFA, MALIMI BUSUNGU ACHANA NAYE… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top