• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 22, 2015

  ‘MTUKUTU’ SULLEY MUNTARI HUYOO UTURUKI, NI BAADA YA ‘KUHARIBU’ AC MILAN

  Muntari ni mchezaji mzuri, lakini ana sifa ya utukutu kuanzia nyumbani Ghana hadi klabu alizochezea Ulaya
  KIUNGO ‘mtukutu’, Sulley Muntari anaweza kutua kwa vigogo wa Uturuki, Besiktas.
  Mkongwe huyo wa Ghana mwenye umri wa miaka 30 alitofautiana na klabu yake AC Milan msimu uliopita na kutemwa akiwa amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake.
  Muntari alijiunga na klabu hiyo kwa mkopo kutoka kwa mahasimu, Inter Milan Januari mwaka 2012 kabla ya soka yake kumfanya apewe Mkataba wa kamili.
  Na tangu ameondoka Milan amekuwa akihusishwa na kuhamia England na Marekani, lakini tovuti ya Sky Sport imeandika, mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana anakwenda Besiktas.
  Muntari ni mchezaji mwenye mafanikio katika ngazi ya klabu na timu za taifa

  Besiktas ipo katika mkakati wa kuboresha kikosi chake, ikiwa tayari imesajili tena winga wake wa zamani, Ricardo Quaresma kutoka FC Porto nab ado inatarajiwa kusajili majina mengine makubwa, akiwemo mshambuliaji wa Ujerumani, Mario Gomez kutoka Fiorentina na Muntari aliyefunga mabao mawili katika mechi 16 za Milan msimu uliopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ‘MTUKUTU’ SULLEY MUNTARI HUYOO UTURUKI, NI BAADA YA ‘KUHARIBU’ AC MILAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top