• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 30, 2015

  SERGE WAWA: NI USHINDI WA KOCHA STEWART HALL

  Serge Wawa amesema ushindi wa jana umetokana na mwongozo na maelekezo mazjuri ya kocha wao, Stewart Hall
  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  BEKI wa Azam FC, Serge Wawa Pascal amesema kwamba ushindi wa jana dhidi ya Yanga SC ni wa kocha wao, Muingereza Stewart Hall.
  Azam jana imetinga Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame zimeyeyuka jana baada ya kupigwa na Yanga SC kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, shujaa wa Azam FC alikuwa ni kipa Aishi Salum Manula aliyepangua penalti ya beki mpya wa kushoto wa Yanga SC, Mwinyi Hajji Mngwali.
  Aggrey Morris akaenda kufunga penalti ya mwisho ya Azam FC na kuzima kabisa matarumbeta na shangwe za Yanga SC Uwanja wa Taifa.
  Penalti nyingine za Azam FC zilifungwa na Kipre Herman Tchetche, Serge Wawa Pascal wote raia wa Ivory Coast, John Bocco na Himid Mao, wakati za Yanga SC zilifungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela na Godfrey Mwashiuya.  
  Na akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE jan baada ya mechi, Wawa alisema kwamba walifuata vizuri mwongozo na maelekezo mazuri ya kocha wao, Hall hadi kufanikisha matokeo mazuri jana.
  “Tulifuata vile kocha alivyotuelekeza na kila mchezaji uwanjani alitekeleza majukumu yake vizuri. Huu ni ushindi wa kocha. Kocha ambaye baada ya muda mfupi ameleta mambo mapya mazuri ndani ya timu,”amesema beki huyo kutoka Ivory Coast.
  Serge Wawa jana ameiongoza Azam FC kuitoa Yanga SC Kombe la Kagame

  Azam FC sasa itamenyana na KCCA ya Uganda katika Nusu ya pili Ijumaa, baada ya Khartoum N na Gor Mahia kupambana katika Nusu Fainali ya kwanza.
  Utamu ni kwamba, Nusu Fainali zote zitakuwa marudio ya mechi za makundi, kwanza Azam FC iliifunga 1-0 KCCA katika mechi ya Kundi C na Khartoum N ilitoka sare ya 1-1 na Gor Mahia katika mchezo wa Kundi A.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SERGE WAWA: NI USHINDI WA KOCHA STEWART HALL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top