KIUNGO Jonas Mkude (pichani) amerejea Dar es Salaam juzi, lakini leo ameshindwa kwenda na wenzake kambini Lushoto, baada ya kutoa udhuru wa siku mbili.
Mkude alikuwa Afrika Kusini kufanya majaribio katika klabu ya Bidvest Wits ya Ligi Kuu ya huko tangu Juni 25 na hakuna majibu yoyote yaliyotolewa hadi sasa kuhusu majaribio yake. Wachezaji wengine wa Simba SC ambao hawakuongozana na wenzao kwenda kambi ya Lushoto ni Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda ambao waliondolewa kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kwa sababu ya majeruhi na kesho watafanyiwa vipimo.
Wengine ni Hassan Isihaka, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Said Ndemla waliokuwa kikosi cha Taifa Stars, ambacho jana kilitoa sare ya 1-1 na wenyeji Uganda, Uwanja wa Nakivubo, Kampala.
Taifa Stars imetolewa Raundi ya Kwanza tu ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani baada ya awali kufungwa 3-0 Zanzibar katika mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita.

.png)
0 comments:
Post a Comment