• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 27, 2015

  MAN UNITED YASAJILI KIPA LA ARGENTINA, VALDES ATUPIWA VIRAGO RASMI

  Kipa Sergio Romero akiwa ameshika jezi ya Manchester United baada ya kukamilisha usajili wake jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  WAPYA WALIOSAJILIWA MANCHESTER UNITED 

  Memphis Depay, PSV - Pauni Milioni 25
  Morgan Schneiderlin, Southampton - Pauni Milioni 25
  Bastian Schweinsteiger, B.Munich - Pauni Milioni 15
  Matteo Darmian, Torino - Pauni Milioni 12
  Sergio Romero - huru
  KLABU ya Manchester United imefanikiwa kumsajili kipa Muargentina, Sergio Romero kwa Mkataba wa miaka mitatu.
  Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 28 alikuwa huru na amechukuliwa kuziba nafasi ya Victor Valdes aliyekuwa kipa wa pili, ambaye sasa anaondoka.
  Romero alicheza chini ya Louis van Gaal klabu ya AZ Alkmaar wakati wanabeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Uholanzi, maarufu kama Eredivisie mwaka 2009 na Muargentina huyo mara moja anaungana na wachezaji wenzake katika kambi ya kujiandaa na msimu nchini Marekani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YASAJILI KIPA LA ARGENTINA, VALDES ATUPIWA VIRAGO RASMI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top