• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 28, 2015

  KHARTOUM N YATAINDIKA APR 4-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KAGAME

  Khartoum N ya Sudan imeifunga APR ya Rwanda mabao 4-0 katika Robo Fainali ya Kwanza Kombe la Kagame mchana wa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  MATOKEO NA RATIBA ROBO FAINALI KAGAME 

  Jumanne Julai 28, 2015
  APR (Rwana) 0-4 Khartoum N (Sudan)
  Gor Mahia (Kenya) Vs Malakia (Sudan Kusini) (Saa 10:15 jioni)
  Julai 29, 2015
  Al Shandy (Sudan) Vs KCCA (Uganda) (Saa 7:45 mchana)
  Azam FC Vs Yanga SC (zote Tanzania) (Saa 10:15 jioni)
  TIMU ya Khartoum N ya Sudan imekuwa ya kwanza kwenda Nusu Fainali ya michuano ya soka ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame 2015, inayoendelea Dar es Salaam.
  Hiyo inafuatia washindi hao wa tatu wa Kundi A, nyuma ya Yanga SC na Gor Mahia, kuifunga APR ya Rwanda mabao 4-0 katika Robo Fainali ya Kwanza mchana wa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mabao ya Khartoum N inayofundishwa kocha Mghana, Kwesi Appiah yamefungwa na Atif Khali dakika ya 10, Amin Ibrahim dakika ya 19 na 36 na Salah Eldin Osman dakika ya 81. 
  Khartoum sasa inasubiri mshindi wa Robo Fainali ya pili kati ya Gor Mahia ya Kenya dhidi ya Malakia ya Sudan Kusini utakoanza baadaye ikutane naye katika Nusu Fainali. 
  Gor Mahia inapewa nafasi kubwa ya kushinda na maana yake itakuwa na mchezo wa marudiano na Khartoum N, baada ya awali kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa Kundi A.
  Robo Fainali nyingine zitachezwa kesho kati ya Al Shandy Sudan dhidi ya KCCA ya Uganda kuanzia Saa 7:45 mchana na baadaye Azam FC dhidi ya Yanga SC, Uwanja huo huo wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KHARTOUM N YATAINDIKA APR 4-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top