• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 22, 2015

  KHARTOUM YAIONYESHA KMKM NJIA YA KUREJEA ZANZIBAR, YAITANDIKA 2-1 TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KHARTOUM N ya Sudan imeionyesha njia ya kurejea Zanzibar KMKM, baada ya kuifunga mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi A, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
  Mchezo huo uliofanyika mchana wa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Khartoum ilipata bao lake la kwanza dakika ya saba kupitia kwa Salah Eldin Osman Bilal.
  Hilo linakuwa bao la tatu kwa Msudan huyo ambaye sasa analingana na Michael Olunga wa Gor Mahia. 
  Beki wa Khartoum N ya Sudan (kushoto), Omer Ali Alkhidr akigombea mpira dhidi ya mshambuliaji wa KMKM ya Zanzibar, Matheo Anthony Simon 

  Beki wa Khartoum N, Samawal Merghani akijivutaa kupiga mpira mbele ya beki wa KMKM, Khamis Ali Khamis. Nyuma kabisa ni Wagdi Awad Abdalla.

  KMKM ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Matheo Anthony Simon dakika ya 58 kabla ya Khartoum N kupata bao la pili kupitia kwa Anthony Akumu Agay dakika ya 84.
  Kharotum inafikisha pointi sita baada ya mechi mbili, wakati KMKM inabaki na pointi zake tatu ilizovuna kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Telecom ya Djibouti.
  Kikosi cha KMKM kilikuwa; Nassor Abdulla Nassor, Khamis Ali Khamis, Juma Mbwana, Pandu Haji Pandu, Said Idrissa Said, Makame Haji Mngwali, Iddi Kambi Iddi, Tizzo  Charless Chomba, Mudrik Muhibu Abdullah, Maulid Ibrahim Ramadhan na Mateo Antony Saimon.
  Khartoum; Mohamed Ibrahim Abdallah, Salah Eldin Osman Bilal, Samawal Merghani, Omer Ali Alkhidr, Hamza Dauwd Zakaria, Antony Akumu Agay, Domenic Abul, Badru Eldin Aldod, Amin Ibrahim Elmani, Wagdi Awad Abdallah na Ahmed Adam Mahmoud.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KHARTOUM YAIONYESHA KMKM NJIA YA KUREJEA ZANZIBAR, YAITANDIKA 2-1 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top