• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 26, 2015

  FM ACADEMIA KUIRUDIA "HADIJA" WALIYOITOA MARA YA KWANZA 1998

  BENDI ya FM Academia “Wazee wa Ngasuma” iko studio kuurudia upya wimbo “Hadija” uliotingisha Tanzania mwishoni mwa miaka ya 90. 
  Saluti5.com wameandika kwamba, rais wa FM Academia, Nyoshi el Saadat amrsema wameamua kuurudia wimbo huo uliorekodiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1998 ili uwe zawadi kwa kizazi kipya cha muziki wa dansi. Nyoshi anasema mashabiki wao wengi wa rika mbali mbali kwa muda mrefu walikuwa wakiomba wimbo huo urudiwe na sasa wameamua kuwapa kitu roho inataka. “Mwaka 1998 tulirekodi wimbo ule kwenye ‘kaseti’ lakini sasa wataupata kwenye tekonolojia za kisasa zaidi huku ukiwa umewekwa pia vinjo vipya ili kuendana na wakati uliopo,” alisema Nyoshi. “Hadija” ni utunzi wake Nyoshi na uliimbwa na bendi hiyo enzi hizo ikijulikana kama FM Musica International ikiwa chini ya Felician Mutta. Wimbo huo ukatesa sana sokoni ukishindana na wimbo “Neema” kutoka kwa bendi ya Diamond Sound “Wana Ikibinda Nkoi” ambayo ilikuwa bendi pinzani kwa FM Musica. Nyoshi anakuwa msanii pekee aliyesalia FM Academia mongoni mwa wanamuziki walioshiriki kurekodi “Hadija” ya mwaka 1998 huku wengi wao wakiwa wametangulia mbele ya haki na wengine kuhama bendi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FM ACADEMIA KUIRUDIA "HADIJA" WALIYOITOA MARA YA KWANZA 1998 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top